KIASI
cha shilingi bilioni 18.77 zimetumwa kwenye akaunti za shule za Msingi
na Sekondari za halmashauri zote hapa nchini kwaajili ya wanafunzi
kusoma bure.
Hayo
yamesemwa na Waziri wa fedha na Mipango, Dk. Philip Mipango wakati
akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
Pesa
hizo zimegawanywa kwenye akaunti za shule za shule za Msingi na
Sekondari katika halmashauri zote kiasi cha shilingi bilioni 15.7 na
bilioni 3 kwenye akaunti vyombo vya usimamizi wa mitihani katika
Halmashauri zote hapa nchini.
Dk.Mipango
amewatahadharisha wakuu wa Mikoa, wakuu wa Wilaya na wakurugenzi wa
Halmashauri zote kutumia ipasavyo pesa hizo kwa kuwa zikitumika kwa
matumizi mengine watalala nao mbele kwa kula jasho la wananchi.
Pia
Waziri wa fedha na Mipango, Dk. Mipango amewaomba waalimu wakuu wa
shule zote za Msingi na Sekondari katika halmashauri zote hapa nchini
waweke wazi matumizi ya fedha hizo katika mbao za matangazo kwa kila
shule ili kila mzazi aweze kujua kiasi gani kimetumika.
Gavana
wa Benki kuu ya Tanzania, Beno Nduru akifafanua jambo kwenye mkutano wa
waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. Kulia Katibu Mkuu wa
wizara ya Fedha na Mipango, Servacius Likwelile.
Kaimu
kamishna mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Alfayo Kidata
akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo,
kuhusiana na ukusanyaji wa mapato katika Malaka ya Mapato Tanzania kwa
kila robo mwaka.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Waziri wa fedha na Mipango, Dk. Philip Mipango jijini Dar es Salaam leo.
Mpekuzi blog
0 comments:
Post a Comment