Saturday, 9 January 2016

Wasiopeleka Watoto Shule Kuburuzwa k=Kortini Machi 30

SERIKALI imesema haitosita kuwafungulia mashtaka na kuwapeleka mahakamani ifikapo Machi 30, mwaka huu, wazazi ama walezi wote watakaoshindwa kupeleka watoto wao shuleni ili kupata elimu ya msingi na sekondari.

Aidha, imepiga marufuku kwa jamii kutumia jina la ‘watoto wa majumbani’, badala yake waitwe wasaidizi hao ‘wasichana wa kazi’ au ‘vijana wa kazi’. Hayo yalisemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, Dar es Salaam jana.

Alisema hayo ili kuhamasisha wazazi na walezi juu ya watoto kujiunga na shule za msingi na sekondari kwa mwaka huu 2016.
Kuhusu kuwafungulia wazazi mashtaka, alisema serikali inaamini kuwa ikiwa inataka kujenga taifa lililoelimika ni lazima kuwekeza kwenye elimu, hivyo ni wajibu wa kila anayehusika kuhakikisha anatimiza wajibu wake.

“Elimu ndio njia bora ya kuwajengea watoto wetu msingi imara wa maisha yao…serikali haitosita kuchukua hatua za kisheria kwa wazazi au walezi ambao watazembea, kumficha, kumtorosha au kuzuia mtoto kuanza masomo ya shule za msingi na sekondari,” alisema Ummy.

Alisema serikali kupitia Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, itawafungulia mashtaka na kuwapeleka mahakamani wazazi na walezi wote watakaoshindwa kutimiza wajibu wao wa kuwapeleka watoto shule, kwani hata Sheria ya Mtoto Namba 2 ya mwaka 2009 Kifungu cha 8, inaelekeza kuwa ni wajibu wa mzazi kuhakikisha mtoto anapata elimu.

Waziri Ummy alisema Kifungu cha 14 kinatamka kuwa ni kosa la jinai, kushindwa kutimiza wajibu huo na adhabu yake ni faini isiyozidi Sh milioni 5 na kifungo kisichozidi miezi 6; au vyote kwa pamoja.

Alisema pia wazazi na walezi, wahakikishe kuwa watoto wanaoendelea na masomo ya shule ya msingi na sekondari, wanahudhuria masomo yao kwa ufanisi, kwa kuwa serikali haitarajii kuendelea kuona utoro wa watoto shuleni kutokana na sababu zinazoweza kuepukika.

Kuhusu kuwepo kwa mwitikio mkubwa wa watoto wanaoanza masomo, alisisitiza kuwa wazazi, walezi na jamii kuhakikisha kila mtoto mwenye umri wa kuanza elimu ya msingi yaani darasa la kwanza na elimu ya awali, kujiunga na shule kwa muda uliopangwa na kuhudhuria masomo ipasavyo.

Kuhusu kuwepo kwa michango mbalimbali katika baadhi ya shule wakati huu wa maandalizi ya shule, alisema serikali imeshatoa mwongozo stahiki. 
Waziri huyo alisisitiza kwamba sio ada peke yake iliyofutwa, bali hata michango yote na tayari serikali imekwishatoa fedha za kugharimia elimu bure na zimekwishapelekwa katika shule zote nchini.

Kwa ujumla, walimu wakuu hawatakiwi kutoza mchango wa aina yoyote, kama vile ya ulinzi, maji, umeme, uzio, fagio, jembe, ndoo na mingineyo, kwani fedha za kugharimia elimu ya bure zitatumika pia kwenye masuala hayo yote

Mpekuzi blog 
Share:

Thursday, 7 January 2016

Rais Magufuli Akutana Na Kufanya Mazungumnzo Na Rais Mstaafu, Benjamini Mkapa Na Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Warioba Ikulu Jijini Dar Es Salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpokea Rais Mstaafu wa Awamu ya tatu, Benjamini William Mkapa Ikulu jijini Dar es Salaam January 7,2016.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 07 Januari, 2016 amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mheshimiwa Benjamin William Mkapa na Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba Ikulu Jijini Dar es salaam.

Akizungumza mara baada ya Mazungumzo hayo Rais Mstaafu Mkapa amesema lengo la kukutana na Rais Magufuli ni kumpongeza kwa dhamana aliyopewa na watanzania kuiongoza nchi, kuunda serikali na kumtakia heri ya Mwaka Mpya.


Rais Mstaafu Mkapa pia amemhakikishia Rais Magufuli kuwa yupo tayari kutoa ushirikiano wakati wote ama kufanya kazi yoyote endapo atahitajika kufanya hivyo.

Kwa upande wake Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba pamoja na kumtakia heri ya Mwaka Mpya, amempongeza Rais Magufuli kwa jinsi alivyoanza kazi vizuri hususani katika kusimamia ukusanyaji wa mapato, kubana matumizi na kuelekeza matumizi kwenye maeneo muhimu ambayo yanawahusu wananchi yakiwemo afya na maji.


Jaji Warioba ameongeza kuwa Watanzania wote wanapaswa kumuunga mkono Rais Magufuli kwa kazi kubwa anazofanya, ambazo ni kukomesha rushwa, ufisadi, matumizi mabaya ya madaraka na wizi wa mali ya umma.

"Lazima kila mmoja amuunge mkono Rais, tusije tukamuachie, pale ulipo kama ni mambo ya rushwa uanzie hapo hapo, kama ni mambo ya matumizi mabaya ya madaraka anzia hapohapo, tusije tukamuachia Rais pekee yake, yeye awe kiongozi wetu, lakini watanzania wote tushughulike na matatizo hayo" alisisitiza Jaji Warioba.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
07 Januari, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpokea Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Jaji Joseph Sinde Warioba Ikulu jijini Dar es Salaam January 7,2016.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Jaji Joseph Sinde Warioba Ikulu jijini Dar es Salaam alipomtembelea January 7,2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Jaji Joseph Sinde Warioba Ikulu jijini Dar es Salaam baada ya kufanya mazungumzo January 7,2016
==>Nini wamekiongea? Tazama Video HII

Mpekuzi blog 
Share:

Mahakama Kuu Kitengo Cha Ardhi Yazuia Jumba la Mchungaji Lwakatare Kubomolewa


MAHAKAMA Kuu Kitengo cha Ardhi imezuia nyumba anayoishi Mchungaji wa Kanisa  la  Assemblies of God Mikocheni, Dk. Getrude Lwakatare kubomolewa.
 
Uamuzi huo wa mahakama ulitolewa juzi na Jaji John Mgeta, baada ya Wakili wa Lwakatare, Emmanuel Muga kuwasilisha maombi ya kupinga ubomoaji huo chini ya hati ya dharura.
 
Jaji Mgeta alizuia ubomoaji wa jengo hilo ama kuchukua hatua yoyote kuhusu jengo hilo lililopo Kawe Beach.
 
Muga aliwasilisha maombi akimwakilisha mdai ambaye ni mtoto wa Mchungaji Lwakatare, Robert Brighton dhidi ya wadaiwa NEMC, Manispaa ya Kinondoni na wadau wengine wote.
 
“Mheshimiwa jaji, nawasilisha maombi ya zuio la kubomoa nyumba ya mteja wangu chini ya kifungu namba 95 cha Sheria ya Mwenendo wa Madai na kifungu namba 2(3) cha JALA vinavyotoa mamlaka kwa mahakama kutoa nafuu stahili pale kunapokuwa na ukiukwaji wa kuvunja haki ya wazi,” alidai.
 
Akitoa uamuzi huo alisema tayari pande husika zilikuwa na kesi namba 70 ya mwaka 2012 na ikamalizika kwa kutoa hukumu na kukazia hukumu iliyompa haki ya ushindi mdai.
 
“Mahakama ilimpa haki mdai, lakini chakushangaza mdaiwa anakiuka matakwa ya hukumu na kutaka kubomoa nyumba, kwa hali isiyokuwa ya kawaida mdai anahitaji ulinzi wa mahakama hii ya haki,”alisema Jaji Mgeta.
 
Alisema nyumba hiyo ipo katika kiwanja namba 2019 na 2020 ambapo hati yake ilitolewa mwaka 1979.
 
Inadaiwa mwaka 2011 NEMC ilitoa notisi ya kuvunja nyumba hiyo baada ya kushinikizwa na wakazi wa eneo hilo wakidai ujenzi wake unaziba Mto Ndumbwi na uko jirani na mikoko.
 
Wakili Muga aliwasilisha maombi ya kuzuia nyumba  ya mteja wake kubomolewa  baada ya Wizara  ya  Maliasili  na  Utalii kupitia  wakala  wa  misitu  Tanzania (TFS ), kuweka alama  ya X wakidai imo katika hifadhi  ya  bahari.

Mpekuzi blog 
Share:

Bilioni 18.77 Zimetumwa Kwenye Akaunti Za Shule Za Msingi Na Sekondari Hapa Nchini Kwa Ajili ya Wanafunzi Kusoma Bure


KIASI cha shilingi bilioni 18.77 zimetumwa kwenye akaunti za shule za Msingi na Sekondari za halmashauri zote hapa nchini kwaajili ya wanafunzi kusoma bure.

Hayo yamesemwa na Waziri wa fedha na Mipango, Dk. Philip Mipango wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.

Pesa hizo zimegawanywa kwenye akaunti za shule za shule za Msingi na Sekondari katika halmashauri zote kiasi cha shilingi bilioni 15.7 na bilioni 3  kwenye akaunti vyombo vya usimamizi wa mitihani katika Halmashauri zote hapa nchini.

Dk.Mipango amewatahadharisha wakuu wa Mikoa, wakuu wa Wilaya na wakurugenzi wa Halmashauri zote kutumia ipasavyo pesa hizo kwa kuwa zikitumika kwa matumizi mengine watalala nao mbele kwa kula jasho la wananchi.

Pia Waziri wa fedha na Mipango, Dk. Mipango amewaomba waalimu wakuu wa shule zote za Msingi na Sekondari katika halmashauri zote hapa nchini waweke wazi matumizi ya fedha hizo  katika mbao za matangazo kwa kila shule ili kila mzazi aweze kujua kiasi gani kimetumika.
Gavana wa Benki kuu ya Tanzania, Beno Nduru akifafanua jambo kwenye mkutano wa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. Kulia Katibu Mkuu wa wizara ya Fedha na Mipango, Servacius Likwelile.
Kaimu kamishna mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Alfayo Kidata akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, kuhusiana na ukusanyaji wa mapato katika Malaka ya Mapato Tanzania kwa kila robo mwaka.
 Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Waziri wa fedha na Mipango, Dk. Philip Mipango jijini Dar es Salaam leo.

Mpekuzi blog 
Share:

Thursday, 31 December 2015

NAWATAKIENI NYOTE HERI YA MWAKA 2016

http://insanityflows.net/wp-content/uploads/2015/12/h2.jpg 

NAWASHUKURUNI SANA KWA SAPOTI YENU 2015 NAOMBENI MUENDELEE KUNISAPOTI 2016.NAOMBENI MNISAMEHE KAMA NILIWAKOSEA NAMI PIA NIMEWASAMEHE.AHSANTENI SANA MUNGU AWABARIKI
Share:

Karibu Mwaka Mpya 2016, Mwaka wa Matumaini Mapya Kwa Watanzania

Mwaka 2016 ni mwaka wa matumaini mapya kwa Watanzania wote walioanza kukata tamaa ya maisha bora. Biashara nyingi zimefilisika kutokana na vikwazo mbalimbali.

Familia nyingi zimeparaganyika kutokana na kukithiri kwa mmomonyoko wa maadili ya kitaifa na kunyauka kwa utu wa ubinadamu uliochochewa na hali duni ya maisha miongoni mwa jamii.

Watu masikini na wenye kipato cha chini wameendelea kukosa mtetezi.

Mwaka 2015, wazee wenye umri zaidi ya miaka 65, ambao hawazidi milioni mbili na nusu hapa nchini, kwa muda mrefu walipaza kilio chao kuhusu haki yao ya msingi ya kupata ‘mrejesho wa hifadhi ya jamii baada ya kulitumikia Taifa lao kwa zaidi ya miongo sita, lakini hakuna aliyewasikiliza.

Huduma za afya ya msingi zilizidi kuwa duni zaidi katika hospitali na vituo mbalimbali vya afya nchini. Kiwango duni cha elimu na mitalaa iliyopoteza mwelekeo, ni baadhi ya vizingiti vilivyoikwaza sekta ya elimu.

Ile dhana ya kikoloni ya kuwalipa wafanyakazi ujira mdogo au mishahara kiduchu au ya kiwango cha chini isiyozingatia utu wa binadamu, iliendelea kukumbatiwa na awamu zilizotangulia.

Kutokana na haya yote, siyo jambo la ajabu , kuikuta Tanzania ikishika nafasi ya 151 miongoni mwa nchi 170 duniani, kwa kiwango cha chini cha hali ya ubora wa maisha ya watu wake.

Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) , katika Ripoti yake ya mwaka 2015 , iliyotoa matokeo ya tathmini za utafiti uliofanyika katika nchi wanachama, ilidhihirisha wazi jinsi ambavyo hata nchi zenye kipato kikubwa zilivyoshindwa kutumia utajiri wake ili kuboresha hali ya maisha ya watu wake.

Utafiti huo uliangazia katika maeneo makuu matatu; huduma za afya, ubora wa elimu na viwango vya mapato.

Nchi nyingi zilizojikuta katika kundi la nchi zenye kiwango cha chini cha ubora wa hali ya maisha ya watu wake, zilitoka bara la Afrika, baadhi yake zikiwa na utajiri mkubwa wa maliasili na rasilimali.

Katika kundi hilo, Kenya ilionekana kuwa na unafuu zaidi kwa kupata kiwango cha 0.548 (HDI) na kuongoza kundi hilo lenye nchi 44.

Nchi iliyoshika mkia katika kundi hilo ni Niger, iliyopata kiwango cha 0.348 , ikilinganishwa na viwango vya juu vilivyoshikwa na nchi ya Norway (HDI 0.944) na Mauritius iliyoongoza katika nchi za bara la Afrika kwa kiwango cha HDI 0.777.

Ripoti hiyo inabainisha pia kwamba katika miaka 25 iliyopita, karibu watu wapatao bilioni mbili kutoka nchi mbalimbali, walifanikiwa kujinasua kutoka katika kundi la nchi zenye kiwango cha chini cha ubora wa hali ya maisha.

Tanzania yenye watu wapatao milioni 45, kuendelea kubaki katika kundi la nchi 44 zenye kiwango cha chini cha ubora wa hali ya maisha ya watu wake, ni kiashiria cha wazi cha kushindwa kwa sera, mifumo na mikakati yake ya matumizi sahihi na makini ya maliasili na rasilimali zake

Kwa mtazamo mwingine ni kwamba, Tanzania ilishindwa kuwa sehemu ya nchi hizo zenye watu bilioni mbili waliofanikiwa kujinasua kutoka katika kundi hilo la ubora wa chini.

Mwaka 2016
Kwa nini mwaka 2016 unaweza kuwa Tumaini Jipya na  mwanzo mzuri wa safari ndefu ya kiuchumi kwa Tanzania?

Matumaini yote ya Watanzania yapo mikononi mwa uongozi wa Serikali ya awamu ya tano.

Kila Mtanzania anatarajia labda uongozi huu utakuja na kitu kipya katika maisha yao, ambacho kilisahaulika kwa miaka mingi. Nacho ni kutokomeza ufukara na umasikini wa kipato kwa vitendo.

Kama miaka 25 iliyopita tumeipoteza bila ya kufikia malengo tuliojiwekea, kutokana na sababu mbalimbali, hatuna sababu tena ya kupoteza miaka mingine 25 ijayo.

Hata hivyo, uongozi mpya wa awamu ya tano, umeanza kuonyesha dalili njema za kukabiliana na adha hiyo.

Serikali ya sasa imerithi uchumi ukiwa katika hali duni na tegemezi, huku taasisi nyingi za umma au za Serikali zikiwa hazifanyi vizuri kama ilivyo kusudiwa. Rushwa na ufisadi navyo vimetapakaa katika kila nyanja ya maisha yetu.

Yote hayo yanafanyika Tanzania ikiwa miongoni mwa nchi chache barani Afrika zilizobahatika kuwa na utajiri mkubwa wa maliasili na rasilimali mbalimbali.

Mtu yeyote aliye na dhamira ya kufunga safari, tena safari ndefu, kwanza lazima ajue wapi anakotaka kwenda. Akisha jua wapi anakotaka kwenda, pili, lazima ajue njia atakayopita na namna ya kumfikisha huko alikokusudia kwenda.

Uongozi mpya wa awamu ya tano, utalazimika kuangalia nyuma tulikotoka (miaka 25 iliyopita). Kisha utafakari, tunaitaka Tanzania ya aina gani miaka 25 ijayo?
Mpekuzi blog
Share:

Jeshi La Polisi Lawatahadharisha Wananchi Kuhusu Mkesha Wa Mwaka Mpya.


TAARIFA YA JESHI LA POLISI KWA VYOMBO VYA HABARI
KUHUSU TAHADHARI KATIKA MKESHA WA MWAKA MPYA   

Tunapoelekea kumaliza mwaka 2015 na kuukaribisha  mwaka mpya wa  2016, wananchi hutumia muda huo kwenda  katika nyumba za ibada ama kusherekea katika maeneo mbalimbali ya starehe, ambapo uzoefu unaonyesha kuwa baadhi ya watu hupenda kutumia fursa hiyo kufanya vitendo  vinavyohatarisha usalama wa raia mali zao.

Jeshi la Polisi nchini, limejipanga vizuri katika mikoa yote kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama ili kuhakikisha kwamba vitendo vyovyote vya uhalifu vitakavyojitokeza  hususani katika kipindi hiki cha kuelekea mkesha wa mwaka mpya vinadhibitiwa. Ulinzi umeimarishwa kwenye maeneo yote ya kuabudia, fukwe za bahari, sehemu za starehe na maeneo mengine yote ambayo yatakuwa na mikusanyiko mikubwa ya watu.

Aidha,  Jeshi la Polisi linatoa tahadhari kwa wananchi wote kuwa makini na kuchukua hatua stahiki za haraka kwa kutoa taarifa pindi wanapoona viashiria vyovyote vya uhalifu katika maeneo yao ya makazi ama maeneo ya biashara. Simu za polisi endapo mwananchi atakuwa na taarifa ni 111 au 112.

 Pia,  Jeshi la Polisi linawatahadharisha wale wote ambao watakuwa wakitumia barabara kuwa makini na kuzingatia sheria za usalama barabarani na hasa kwa madereva wa magari na pikipiki, kuepuka kujaza watu kupita kiasi, kwenda mwendo kasi, kutumia vilevi pamoja na kupiga honi hovyo.

Vilevile, wananchi kuacha tabia ya kuchoma matairi barabani pamoja na kupiga mafataki. Aidha, yeyote atakayefanya vitendo hivyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

Nawatakieni watanzania wote kheri ya mwaka mpya.
Imetolewa na:
Advera John Bulimba-SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.

Makao Makuu ya Polisi. 
Share:

AHSANTE SANA KAKA ANTONY LUVANDA

 
Moja ya Mtu amabaye amechangia kwa kiwango kikubwa kupitia motivations na inspirations zake.Ahsante sana kaka ubarikiwe mc Luvanda Antony
Share:

MC EDWIN LUVANDA ALIUFANYA USIKU WA SEKION DAVID (SEKI) NA REHEMA UFANE SANA IFAKARA MOROGORO

Muigizaji na Mtayalishashaji wa Kundi la The Original Comedy Sekion David na Rehema wakiwa katika nyuso za furaha katika kusherekea harusi yao baada ya kuuaga ukapera.Sherehe iliyofanyika jana 3 oktoba 2015 katika ukumbi wa bustan za bethelem ifakara,Morogoro
 Bwana harusi Sekion David (Seki) akimtambulisha mkewe Rehema

Edwin Luvanda majina yake ya kwenye passport maarufu kwa jina la MC EDWIN LUVANDA akiwajibika kuhakikisha wageni waalikwa wanafurahi mwanzo mwisho



Bibi harusi Rehema akimtambulisha mume wake Seki
   Mchekeshaji Joti wa ze comedy akiwa na furaha baada ya mtayarishaji wao Sekion David maarufu kwa jina la Seki kuuaga ukapera 


Mchekeshaji Wakuvwanga akitoa lake la moyoni kwa seki ambaye ni mtayarishaji wao wa ze comedy.Kushoto wa kwanza ni Joti wa pili ni Mac Regan wa ze comedy


 
Bwana Harusi Seki akiwa na Best Man wake



Maharusi wakiwaaga wageni waalikwa tayari kuondoka ukumbini
Maharusi wakiwa wanaondoka ukumbini

Mc Edwin Luvanda  nakutakia maisha mema ya ndoa kaka Seki tumefarijika kufanya kazi na wewe.
Share:

INNER PARTY YA HARUSI YA SEKI WA ZECOMEDY ILIFANA SANA MIRADO HALL DAR

Mapokezi ya Sekion na Rehema  Mirado hall Sinza

 
Inner party ya harusi ya Seki iliyofanyika Ifakara Morogoro
 
Seki na mke wake wakifurahia jambo
 
  
MC Edwin Luvanda kulia pamoja na Mpoki kushoto
Share:

USIKU WA SEND OFF YA DORIS NDAWI UKUMBI WA MATTI IGURUS MBEYA

 
Share:

MATUKIO MAPYA


Recent Posts Widget

MAKTABA YETU

BLOGS RAFIKI

Powered by Blogger.